Languages

JOPO LA KISWAHILI

“NYOTA YA UFANISI”

Kiswahili ni chemichemi ya utangamano na utamgusano thabiti wa kila jumniya. Fahari ya mwaafrika halisi. Ukidalalisha thabiti wa Kiswahili wajidalalisha mwenyewe na uzawa wako
Kiswahili ni chombo cha maendeleo ya nchi yetu; kumbuka China, Ureno na hata Tanzania. Tuionee fahari Lugha ya Kiswahili ambayo ni maarufu na enezi si haba. Hadhi tuikuze na elimu iwe malighafi kwa ustawi wa uchumi wetu. Chekechea hadi vyup vikuu, Kiswahili kiwe nguzo stadi. Jivunie lugha yako staarabika uimarike.

TAMKO LA BUSARA

“Haijalishi kasi ya mwendo, mradi tu hatukomi.”
“Ubabe si ugwiji; uafahamu ni ngumu.”
“wasomi husomani iwapo hekima haidhihiriki.”
“mkono hukulishao hukatwi.”
Bw. Sianyo E.
(Baba ameketi hapo nje anamwita mtoto)
Baba naomba uniletee soda
Mtoto: Cocacola au Sprite?
Baba: Cocacola
Mototo: Baridi au moto?
Baba: Baridi
Mototo: Kwa glasi au na straw?
Baba: Aaargh!………….wachana nayo, unipe maji
Mototo: Baridi au moto?
Baba: Baridi.
Mototo: Chemshwa au la?
Baba: Yaliyochemshwa
Mototo”: Kwa glasi au kikombe cha chai?
Baba: wewe mtoto nitakuuwa saa hii
mtoto: kwa bunduki au kisu?
Baba: Toka hapa sitaki kukuona
Mtoto: Saa hii au baadaye
Baba: Heri tungekuzaa kama maziwa mtindi……………….
Mtoto: Daima au yeyote?
(Huyu mtoto angekuwa wako ungemfanyia nini?)
By. Joy Simiyu

UCHAGUZI WA MATATA

Kwa jina lake muumba, hakika natanguliza, Kukicha mie naomba, bila yeye singeweza, Kwa mambo yalotukumba, kikumbuka yaniliza
Uchaguzi wa matata, lioleta uhasama, kila mtu katwakata, Baba kaka hata mama, Kila mahali matata, mbili na saba elfu, uchaguzi wa matata
Kila nikumbukapo, machozi hububujika, Kila nifikiriapo, viungo hutetemeka, Mbili na saba elfu, uchaguzi wa matata
Vituko vilitokea, matokeo kutangzwa, Watu walioshtukia, ushindi katawazwa, wengine walitulia, wengine walikwaazwa, mbili na saba elfu, uchaguzi wa matata
Nyumba zilibomolewa, mali yakaharibiwa, Na watu waliuliwa, na wengine kughasiwa, wengine waliobakiwa na upweke na ukiwa, mbili na saba elfu, uchaguzi wa matata
Mambo yaliotokes, kweli yalikuwa kisa, na pole kuwaambia ndilo tunaloliweza, na sisi waliobaki, amani twasisitiza, mbili na saba elfu, uchaguzi wa matata
Yaliyopita si ndweli, Kenya tugange yajayo, Katu tusibaki pale, pa vurugu na miayo, daima tusonge mbele, kusahau mambo hayo, Mbili na saba elfu, uchaguzi wa matata
Na Asha Omar

‘MKONO INUKA’

Mkono inuka, inuka hima twaa kalamu

Upate ya’ndika, kwa hati njema hino nudumu

Ipate someka, wenye kusoma waifahamu

Wapate yashika, na kuyapima yaliyo humu

 

Kuandika anza, anza sikawe mkono wangu

Na mimi naanza, kisa chenyewe cha mlimwengu

Alivyonifunza, nao wajue waja wenzangu

Wapate jitunza. Salama wawe hawa ndugu zangu

 

Mja hana haya, haya hazima mwake usoni

Mja ni mbaya, hutimba shimo ingiye ndani

Na ukishangiya azame zomo furaha gani

Mmoja kwa miya, ndiye hayumo baya kundini

Contact Information
H.O.D Kiswahili
Stay in Touch